Cristiano Ronaldo alimuacha mtoto mdogo shabiki wa klabu ya Bournemouth akiwa amevunjika mkono kutokana na shuti lake la mita 35 lilotokana na faulo wakati wa wa mchezo wa Real Madrid dhidi ya timu hiyo inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza nchini England.
Charlie Silverwood, 11, alikuwa mmoja ya washabiki waliobahatika kuwepo kwenye uwanja wa Dean Court kuangalia mechi hiyo - alikuwa amekaa siti ya pembezoni mwa goli la Bournemouth wakati nahodha wa Ureno alipokuwa akipiga faulo ya umbali wa mita 35.Na Shaffih Dauda
Ronaldo akipiga faulo iliyoenda kusababisha kuvunjika mkono kwa Charlie |
Baba yake Charlie aliona hatari ya shuti la Ronaldo na akaweza kulikwepa shuti la Ronaldo, lakini akakutwa na uzito wa shuti hilo kwenye mkono wake, na kuacha kiganja chake kikiwa kimevunja mara mbili.
Pamoja na maumivu makali, Charlie hakutaka kukosa kumuangalia kipenzi chake Ronnie na akaendelea kuangalia mpira mpaka dakika ya 84 ndio akaelekea hospitali, ambapo ndipo alipofahamu uharibifu uliofanywa na shuti la Ronaldo kwenye mkono wake.
Charlie alipigwa X-ray na akatakiwa kufanyiwa uapasuaji kabla ya mkono wake kuwekwa P.O.P ambalo atakaa nalo kwa wiki sita.
Lakini kuliko kuacha maumivu yake yasimfanye kuweza kuonana na mastaa kama Gonzalo Higuain, Luka Modric na Mesut Ozil alijikaza na kurudi maeneo ya Dorset, kujaribu kuonana na mastaa wake.
‘Niliumia sana,’ Charlie aliiambia The Sun. ‘Nimewambia marafiki zangu na hawaamini. Ronaldo ndio mchezaji ghali zaidi duniani - na amenivunja mkono wangu.
‘Niliuona mpira ukinijia mbele yangu, Uliupunyua mwamba na kupita na ulikuwa unakuja kwenye uso wangu - hivyo niliamua kuuzuia na mkono. Baba yangu alikuwa karibu na mie na akaukwepa na hivyo wote ukanikumba mie kwa nguvu zote.’
Baada ya mchezo huo klabu ya Bournemouth ilimpa jezi iliyosainiwa na wachezaji wa Real Madrid pamoja na mpira.
No comments:
Post a Comment