Mtuhumiwa huyo akiwa kwenye ofisi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Karume
kata ya Mnadani wakati alipokuwa akihojiwa kuhusu tuhuma yake ya
kumjeruhi mtoto wake kichwani na mgongoni.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Karume kata ya mnadani manispaa ya Dodoma Matwiga Kyata
akionyesha moja ya majeraha ya kichwani na Mgongoni, aliyojeruhiwa mtoto
MaggE Fred 8, kipogo hicho kinadaiwa kufanywa na mama yake mzazi.
MTOTO Magge Fred 8 amejeruhiwa
kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi
kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.
Magge alisema anajisikia maumivu makali kichwani na mgongoni
baada ya kupigwa na mama yake mzazi kutokana na madai ya yeye
kutomwambia Dada yake alipo na chips ambazo mama yake alizikuta chini ya
mvungu wa kitanda
tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jumanne hii, inadawa kuwa Theresia Fidelis ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alimpiga na kumjeruhi mwanae, mwandishi wetu alishuhudia kovu kichwani la kipigo cha kitu kilichomchana na huku mgongoni kukiwa na majeraha kadha ya meno ambavyo vimemsababishia maumivu makali.
Akiongea mbele ya Mwenyekiti wa mtaa mama wa mtoto
huyo alisema aliamua kumpiga kiasi hicho kutokana na mtoto huyo
kumfichia siri Dada yake na pia kuiba fedha ndani na kununua chipsi
pamoja na matumizi mabaya ya anasa.
Theresia alisema imekuwa ni kawaida kwa mtoto wake huyo
Magge Fred 8 kutosema Dada yake alipo na fedha zinazopotea ndani
kutojulikana aliyechukua badala yake anaona chipsi na vitu vingine
vidogo vidogo vya anasa ndiyo sababu ya kumpiga vibao mpaka kujigonga
ukutani na kuchanika kichwani na kumng'ata kutokana na hasira.
.
.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume kata ya Mnadani Matwiga
Kyata alisema tukio hilo lililpofikishwa ofisini kwake aliamua kuchukua
hatua za kisheria na baada ya mahojiano aliamua kuwaita polisi ili
sheria ikachukue mkondo wake zaidi.
Baadhi ya akina mama waliokuwepo ofisini hapo kushuhudia
tukio hilo walisema mtoto huyo alikimbia toka kwa nyumbani kwao usiku
huku akilalama kutaka kuuawa ndipo waka mpeleka kwa mwenyekiti, pamaja
na kulaani kitendo alichofanya mwanamke mwenzao.
''We acha hivi unajua uchungu tunaoupata wakati wa
kujifungua? kama kweli aliupata angeweza kufanya hivi mpaka kufikia
kumng'ata meno akitaka kumnyofoa nyama mtoto wake wala haiingii akili
labda akapimwe akili la sivyo achukuliwe hatua kali zinazostahili'',
alisema Mwatum Rashid.
Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka
wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona watoto wakifanyiwa vitendo
viovu na wazazi au walezi wao.
No comments:
Post a Comment