Muonekano wa ndani ya duka hilo.
Mwaija Salum na Chande Abdallah
HII kali! Oparesheni Fichua Maovu a.k.a OFM inazidi kufukunyua vya
kufukunyuka, safari hii ikikutana na kioja cha aina yake ambapo ilinasa
duka la kuuza dawa za binadamu ‘pharmacy’ likifanya biashara nyingine
tofauti na hiyo.
Mnyetishaji wetu ambaye hakupenda jina lake liandikwe, alitonya kuwa duka hilo linapatikana Hananasif, Kinondoni, Dar es Salaam.
Timu ya
OFM ilivamia eneo hilo na kujiridhisha ambapo ilishuhudia bidhaa
nyingine kama mbogamboga, nazi, ndizi, vitunguu, nyanya na mazagazaga
mengine rafiki kwa mama yakiuzwa ndani ya duka hilo.
Cha kushangaza zaidi, pia ndani ya duka hilo la kuuzia dawa muhimu,
kulikuwa na jiko la kupikia likiendelea kutekeleza majukumu ya
kukaangiza kama kawaida. NA GLOBAL PUBLISHER
Mariam Seleman ambaye ni mmiliki wa duka hilo.
Timu yetu
ilifunga safari hadi kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Hananasif, Suleiman Lada
na kumweleza juu ya tukio hilo ambapo iliungana naye hadi dukani hapo na
kujionea jambo lililomshangaza na kusema: “Sikufahamu kabisa kama kuna
kitu kama hiki mtaani kwangu.
“Lakini
nitafuatilia hili suala kisheria nione, lazima afuate taratibu
zilizowekwa na wizara (ya afya) katika kuuza dawa za binadamu,
vinginevyo hili duka nitalifunga.”
Baadhi ya bidhaa zilizopo katika duka hilo.
Muuzaji wa
duka hilo ambaye ndiye mmiliki aitwaye Mariam Seleman, alisema hajui
kama kuna sheria inambana kutochanganya biashara hiyo na mahitaji
mengine.
“Kiukweli
mimi nilikuwa sijui kama ni kosa kufanya hivyo ndiyo maana nimeuza hapa
kwa mwaka mzima na sijawahi kuulizwa na mtu yeyote. Hata hivyo kwa
sababu leo mmenielewesha basi itabidi nichague biashara moja ya kufanya
kama ni dawa au vyakula,” alisema Mariam.
No comments:
Post a Comment