Pages

Tuesday, July 9, 2013

Matukio mbalimbali ya Waziri Mkuu Pinda akiwa ziarani Iringa na Njombe.


IMG_0928
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsaidia kutembea mtoto, Asante Mtega wa kituo cha kulea na kuwasaidia watoto wenye ulemavu cha cha Inuka kilichopo  Mayale Iringa wakati alipokitembelea  Julai 8,2013. Katikati ni Mkewe Tunu na Kushoto ni Askofu wa kanisa Katoliki Njombe, Alfred Maluma. (picha na Ofisiya Waziri mkuu).
IMG_0957
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa  Kijiji cha Igwachanya  wilayani Wanging’ombe  wakati alipoingia kijijini  hapo akiwa  katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 8, 2013. Kushoto ni Mkewe Tunu na Kulia ni mkuu wa Wilaya hiyo Estelina Kilasi.
IMG_0983
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Alfred Maluma wakiweka jiwe la msingi la Chuuo cha Kilimo na Mifugo cha Mare- Mayale , Katika wilaya ya Wanging’ombe. Jana.  kulia ni mkewe Tunu Pinda.
IMG_1032
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe,Alfred Maluma  kabla ya kuwaslimia wananchi  katika misheni ya Ilembula wilayani Wanging’ombe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe leo.

No comments:

Post a Comment