Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr
Christine Ishengoma akitoa heshima ya mwisho katika mwili wa marehemu
Koplo Owald Chaula leo
Wanajeshi wakiuandaa mwili wa mwenzao
Wananchi na ndugu wa Chaula wakilia kwa uchungu |
Wananchi wakitoa heshima zao za mwisho
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald
Guninita kutoka kushoto ,mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Ishengoma na
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Sety Mwamoto pamoja na kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi wakiwa katika msiba huo
DC Kilolo Bw Guninita akitoa heshima zake akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM Kilolo SEty Mwamoto
Mwili wa askari Chaula ukielekea makaburini
Mwili huo ukishushwa kaburini
Heshima za mwisho za kijeshi kwa marehemu Koplo Oswald Chaula
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Ishengoma akiweka shada la maua
DC Kilolo akiweka shada la maua katika kaburi hilo la marehemu Chaula leo
Mwakilishi wa JWTZ akiweka shada la maua
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita akiwafariji wafiwa
Mwenyekiti wa CCM Kilolo Bw Sety
Mwamoto wa tatu kulia akiwa na viongozi wenzake katika mazishi hayo
picha na Said Ng'amilo na Francis Godwin wa matukiodaima.com
.................................................................................................................................................
MKUU wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma
leo aongoza mamia ya wakazi wa
wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa katika mazishi
ya askari mmoja kati ya
askari 7 wa jeshi la
wananchi Tanzania (JWTZ) waliouwawa katika shambulio la ghafla Darfur nchini Sudani marehemu Coplo Oswald Chaule .
Mkuu huyo wa
mkoa akiwa ameongozana na viongozi
mbali mbali wa chama na
serikali katika wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa ameongoza mazishi hayo katika kijiji
cha Mtitu wilaya ya Kilolo
,huku akitoa ubani wa Tsh 200,000 wakati mkuu wa
wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akiwasilisha rambi rambi ya wananchi
na watumishi wa
Kilolo la Tsh 300,000 kwa familia ya
askari huyo.
Akitoa salam za rambi
rambi mkuu huyo wa mkoa alisema
kuwa mkoa wa Iringa na Taifa limepoeza askari shupavu ambao
wataendelea kukumbukwa kutona na mchango wao katika
Taifa .
“ Mkoa wa Iringa umeondokewa na kijana
shupavu na mzalendo katika Taifa
lake ambae alijitoa kwa
ajili ya kulitumikia Taifa ….hivyo
sisi kama serikali ya mkoa tutaendelea
kumuenzi marehemu kwa uzalendo
wake katika taifa”
Mazishi ya wanajeshi
hao yanafanyika huku
ikiwa imebaki siku
moja kwa Taifa
kuadhimisha siku ya mashujaa nchi
ambapo katika mkoa wa Iringa
maadhimisho hayo hufanyika katika viwanja
vya bustani ya manispaa ya
Iringa .
Wakizungumzia juu
ya kifo
cha mwanajeshi huyo baadhi ya
viogozi wa vyama
vya siasa na serikali akiwemo mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Kilolo Sety Mwamoto alisema kwa
vifo vya wanajeshi
hao vimelitikisa Taifa na kuwa
mchango wao katika Taifa
utakumbukwa daima.
PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment