MFANYABIASHARA
maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed
Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City
Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu
zaidi.
Hali
yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake
moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili
liko salama.
Wiki
iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa
tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda
tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu
kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.
Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.
Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.
Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment