Pages

Friday, July 5, 2013

POLISI WAVAMIA NYUMBANI KWA MJUKUU WA MANDELA KUSAKA MABAKI YA MIILI...


KUSHOTO: Mandla Mandela. KULIA: Msafara wa maofisa wa polisi pamoja na gari la kubebea maiti wakielekea kusaka miili nyumbani kwa Mandla huko Mvezo.
Polisi wa Afrika Kusini wamevamia nyumbani kwa mjukuu wa Nelson Mandela kusaka miili mitatu anayodaiwa kuihamisha kinyume cha sheria.
Hii imekuja baada ya Mandla Mandela juzi kushindwa kesi mahakamani dhidi ya ndugu 16 wa familia yake ambao wanamtuhumu kwa kuhamisha miili hiyo ya watoto watatu wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini bila idhini yao.

Mahakama ya Mthatha iliamua kwamba mabaki hayo yarejeshwe katika eneo ya maziko la familia hiyo hadi kufikia juzi Saa 9 alasiri.
Askari wa Mahakama walivamia milango ya kuingia nyumbani kwake huko Jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini wakiwa na mashoka kabla ya maofisa wa polisi kufukua ardhini kusaka miili hiyo. Magari matatu ya kubebea maiti mazikoni pia yalionekana kwenye eneo hilo, gazeti la Eyewitness News la Afrika Kusini liliripoti.
Familia hiyo ilimburuta Mandla mahakamani baada ya kuzika upya mabaki ya miili katika eneo lake alikozaliwa la Mvezo mwaka 2011.
Ndugu wa Mandela walidai kwamba Mandla hakuwa na ruhusa au hata kuwataarifu wanafamilia wakati akifanya maamuzi hayo.
Ndugu wa Mandla wamesema kwamba nafasi yake kama chifu wa kijiji hicho sasa iko hatarini

No comments:

Post a Comment