Pages

Friday, August 16, 2013

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MABALOZI WA DJIBOUTI,BENIN NA CAMBODIA AKIWEMO MKURUGENZI MTENDAJI WA EXIM BANK TANZANIA LTD

Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico alipokutana na Mhe. Roble Olhaye, Balozi wa Djibouti nchini Marekani na ambaye pia ni kiongozi wa Mabalozi wa
Afrika
 
wanaoziwakilisha nchi zao hapa Marekani (Dean of Diplomatic Corps). Katika mazungumzo yake Mhe. Balozi Olhaye alitumia muda mwingi kumweleza Mhe. Balozi Mulamula uzoefu wake kama Balozi nchi humu pamoja namna Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inavyofanya kazi zake za kidiplomasia na nini ategemee katika mwenendo mzima wa shughuli za Serikali ya Marekani inaposhughulikia masuala yanayohusu nchi zao mbili. Balozi Olhaye pia alimshauri Balozi Mulamula mambo mengi ya msingi katika kufanikisha majukumu yake ya kikazi kwa muda wote akiwa hapa Marekani. Aidha, Balozi Olhaye ambaye amekuwa Balozi wa Djibouti nchi Marekani tangu tarehe 22 Machi,1988 na hivyo kuwa ni Balozi anayeiwakilisha nchi yake kwa muda mrefu kuliko Balozi mwingine yeyote nchi Marekani kwa miaka 25 sasa alimtakia Mhe.Balozi Mulamula kila la kheri katika majukumu yake mapya.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mhe. Cyrille Oguin wa Benin alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Balozi huyo ambaye ni kiongozi wa Mabalozi wa nchi za Jumuia ya ya Uchumi ya Magharibi mwa Afrika ( ECOWAS).
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mhe. Hen Heng, Balozi wa Cambodia nchini Marekani alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Balozi huyo ambaye ni kiongozi wa Mabalozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia(ASEAN)
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Bw.Anthony Grant, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Limited alipofika Ubalozini Tanzania House,Washington DC kumsalimia na kumweleza madhumuni ya ujio wake nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment