Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico alipokutana na
Mhe. Roble Olhaye, Balozi wa Djibouti nchini Marekani na ambaye pia ni
kiongozi wa Mabalozi wa
Afrika
wanaoziwakilisha nchi zao hapa
Marekani (Dean of Diplomatic Corps). Katika mazungumzo yake Mhe. Balozi
Olhaye alitumia muda mwingi kumweleza Mhe. Balozi Mulamula uzoefu wake
kama Balozi nchi humu pamoja namna Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
inavyofanya kazi zake za kidiplomasia na nini ategemee katika mwenendo
mzima wa shughuli za Serikali ya Marekani inaposhughulikia masuala
yanayohusu nchi zao mbili. Balozi Olhaye pia alimshauri Balozi Mulamula
mambo mengi ya msingi katika kufanikisha majukumu yake ya kikazi kwa
muda wote akiwa hapa Marekani. Aidha, Balozi Olhaye ambaye amekuwa
Balozi wa Djibouti nchi Marekani tangu tarehe 22 Machi,1988 na hivyo
kuwa ni Balozi anayeiwakilisha nchi yake kwa muda mrefu kuliko Balozi
mwingine yeyote nchi Marekani kwa miaka 25 sasa alimtakia Mhe.Balozi
Mulamula kila la kheri katika majukumu yake mapya.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula
akisalimiana na Mhe. Cyrille Oguin wa Benin alipokwenda kujitambulisha
rasmi kwa Balozi huyo ambaye ni kiongozi wa Mabalozi wa nchi za Jumuia
ya ya Uchumi ya Magharibi mwa Afrika ( ECOWAS).
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa
na Mhe. Hen Heng, Balozi wa Cambodia nchini Marekani alipokwenda
kujitambulisha rasmi kwa Balozi huyo ambaye ni kiongozi wa Mabalozi wa
nchi za Kusini Mashariki mwa Asia(ASEAN)
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa
na Bw.Anthony Grant, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania
Limited alipofika Ubalozini Tanzania House,Washington DC kumsalimia na
kumweleza madhumuni ya ujio wake nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment