Kuna
barua nyingine tena zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa wa Kitanzania
wanaotumikia vifungo vyao huko Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya
kulevya. Anayechapisha barua hizo kwenye mitandao anadai eti ni za
kweli na zinatoka kwa wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani huko
Hong Kong. Anadai kuwa yeye ni padri na huwa anaendesha ibada
magerezani. Anadai huwa anatembelea magereza ya Hong Kong karibu kila
siku ambapo hukutana na wafungwa wa Kitanzania.
Naomba
nimnukuu kama alivyoandika yewe mwenyewe baada ya mchangiaji mmoja
kwenye tovuti husika kumhoji kuhusiana na ukweli wa hizo barua.
Letter is 100% genuine, like the previous
letters. And there’s more to come. I am a Catholic priest, a prison
chaplain. I visit Hong Kong prisons almost every day and often see the
Tanzanian inmates. They are deeply upset that they will not see they
families for many long years and that their families are suffering
because of their imprisonment. I am trying to help others avoid the same
fate ….as well as trying to help protect Hong Kong society from drugs. I
also visit local drug addicts in prison ….the other side of the coin
….and I see the severe damage that has been done to their minds and
bodies. This is a totally lose-lose situation and must be stopped
Kuhusiana
na wafungwa wa madawa ya kulevya huko Hong Kong Balozi Marmo alishawahi
kusema kuwa idadi ya Watanzania walio katika magereza na mahabusu huko
China, Hong Kong na Macao, inatisha. Alipoulizwa hatima ya Watanzania
hao, Balozi huyo amesema, “Tunawapa ushauri nasaha kwa sababu kuna
udanganyifu mkubwa kwenye magereza hayo (walimofungwa), wengine
wanaambiwa kwamba kuna uwezekano wa kuwarejesha nyumbani ili wamalizie
vifungo vyao, lakini huwa tunawaambia hili jambo haliwezekani kwa sababu
Tanzania na China, Tanzania na Hong Kong na Tanzania na Macao hatuna
mikataba ya kubadilishana wafungwa.
“Na
wala hatuna sasa hivi uwezekano wa kufanya jambo hili kwa sababu mzigo
ni mkubwa, laiti ingepita miaka miwili au mitatu bila kuwa na mtu au
mhalifu wa kuleta dawa za kulevya, tungekuwa na mjadala na mataifa
haya.” Anasema Balozi Marmo, “Kunakuwa na uchunguzi mkali sana,
unachukua wakati mwingine hadi miaka mitatu. Hujui (hao watuhumiwa)
wanazielezea nini mamlaka za hapa.”Zipo
barua tatu. Barua ya kwanza inadaiwa kuandikwa na mfungwa Agosti 9,
2013 kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete. Barua ya pili haina tarehe. Barua
ya tatu inadaiwa kuandikwa Agost 8, 2013 kwenda kwa Dr. Mwakyembe na
imeoothoresha majina ya wanaodaiwa kuhusika na biashara ya madawa ya
kulenywa, yakiwemo majina ya viongozi wa kidini. Again, sina uhakika
kama waliotajwa wanahusika na hiyo biashara. Mie nimekopi na kupaste tuu
habari kama nilivyoikuta. kama yaliyoandikwa kwenye hizo barua ni ya
kweli au uongo kwa kweli ni vigumu sana kujua.
jamiiforum
No comments:
Post a Comment