Pages

Thursday, August 15, 2013

HII NI HATARI KWA TAIFA::TINDIKALI YAUZWA KWEUPE.......



Chande Abdallah na Hans Mloli

LICHA ya serikali kutangaza kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kimiminika hicho bado kinapatikana kirahisi mitaan

Mwishoni mwa wiki iliyopita, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele walitoa tamko la kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali ambao umesababisha kujeruhiwa kwa watu wengi nchini.

Jumatatu iliyopita, mapaparazi wetu walizama mitaani na kuanza kuisaka bidhaa hiyo ili kuona kama upatikanaji wake una ugumu wowote.
 

Katika maabara moja iliyopo Kinondoni, Dar mapaparazi waliambiwa tindikali inapatikana, nusu lita shilingi 45,000. Maabara moja iliyopo Ilala, bidhaa hiyo inapatikana kwa nusu lita shilingi 30,000, lakini bei inaweza kupungua hadi shilingi 25,000.
 

Mapaparazi hawakuishia hapo, walifika hadi Kipawa jijini Dar ambapo walikutana na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ambaye alisema anaiuza bidhaa hiyo kwa shilingi 16,000 tu na hashushi zaidi ya hapo. Tindikali hiyo ni mali ya shule. Zoezi la kuiandaa likaanza ambapo mwalimu huyo alikuwa akichanganyachanganya malighafi na kupata tindikali kamili.

Ili kuithibitisha kuwa ni tindikali kweli, aliwapa mapaparazi makaratasi maalum (litmus paper) ambayo hutumiwa kufanyia ‘test’ kitaalam. Makaratasi hayo hubadilika rangi toka bluu kuwa mekundu kila yanapokutana na tindikali na kuashiria kuwa ni yenyewe. Wakati akiendelea kuchanganya, mara kadhaa wanafunzi waliingia lakini aliwatoa nduki.

Huku akirekodiwa video kwa siri (ipo Global), mwalimu huyo alisema amekuwa akiwauzia watu mbalimbali bidhaa hiyo na alikiri kwamba huwa hawaulizi wanakwenda kufanyia nini kama ambavyo hakuwauliza mapaparazi wetu.
 

Hadi mapaparazi wetu wanaondoka shuleni hapo, mwalimu huyo hakujua kama wanunuzi waliokwenda kununua tindikali hiyo ni ‘wapelelezi’ mahiri kutoka Global Publishers.  Mitaani watu wanasema tindikali ni silaha mpya ya maangamizi kwa kizazi cha sasa ambapo kila kukicha hofu ya watu kujeruhiwa na kimiminika hicho inazidi kupanda.
 

Mpaka sasa, Watanzania wengi wameshamwagiwa tindikali na watu wanaosadikiwa ni wabaya wao. Miongoni mwa watu waliokumbwa na balaa hilo ni mmiliki wa Home Shopping Center, Said Mohamed Saad, Shehe wa Bakwata wilayani Arumeru, Issa Makamba na mtu  aliyedaiwa ni mpiga debe wa CCM, Igunga  Mussa  Tesha.
 

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Katibu wa Mufti Zanzibar, Shehe Fadhili Soraga na wasichana wawili raia wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee.Chanzo;GLOBAL PUBLISHERS BLOG

No comments:

Post a Comment