Waziri
wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira,Dkt. Terezya Huvisa
akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake jijini dar es salaam leo
kuhusu tamko la serikali la upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya
plastiki hapa nchi.
(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Serikali
imepiga marufuku ungizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko
ya plastiki. hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa
Rais(mazingira) Dk Terezya Huvisa alipokuwa akizungumza na waandishi
ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Dkt.
Hufisa ameeleza kuwa Serikali imehamua kuchukua hatua hii ili kupunguza
ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko
ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa
mazingira .
Alisisitiza
kuwa, Zuio hili linahusu mifuko yote ya Plastiki ya kubebea bidhaa toka
madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni
mia moja inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbali
mbali kama vile vifaa vya mahospitalini.
“Marufuku
hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi kwa
ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya
plastiki kwenye mazingira.” Alisema.
Dkt
Hufisa aliendela kusema kuwa, Jitihada zinatakiwa zifanywe ili
kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa, na misako ya watu wanaofanya
biashara ya mifuko hii ifanyike katika maeneo yote ndani ya nchi yetu,
na watakaokiuka wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kufanikishwa
katika vyombo vya sheria .
Imeelezwa
kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na
uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo
kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama ,kutooza kiurahisi
wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa,
bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi
katika mazingira.
No comments:
Post a Comment