Pages

Friday, August 16, 2013

HUYU NDO PAULO HENRIQUE,MGONJWA WA KUPOOZA ANAYEISHI HOSPITALI KWA MIAKA 45 SASA

                                  Paulo Henrique

Paulo Henrique Machado, raia wa Brazil ameishi hospitalini kwa kipindi cha miaka 45 sasa kutokana na kupooza kulikosababishwa na ugonjwa wa polio alioupata baada ya kuzaliwa na mama yake kufariki.

Paulo na watoto wengine walipatwa na ugonjwa huo baada ya kutokea mlipuko nchini

humo miaka ya 70, na tangu wakati huo, Paulo amekuwa akipumulia mashine saa 24 kwa siku, huku watoto wenzake wengi wakiaga dunia miaka michache baadaye.
Pamoja na masaibu mengi aliyoyapitia, yote hayo hayajawa kikwazo cha kumzuia Paulo kutumia ubongo

na akili yake kwani ameweza kupata elimu na kubobea katika masuala ya utengenezaji vikaragosi/vibonzo kwa kutumia kompyuta (computer animator) na sasa ameanza kutengeneza tamthiliya kuhusu maisha yake inayotokana na kitabu kilichoandikwa na rafiki yake --ambaye pia ni mgonjwa, Eliana-- ambayo itaonekana kwenye runinga.

Anatamani sana angeweza kucheza soka kama watoto wengine, lakini kwa kujikubali kuwa haiwezekani, ameweza kutumia akili yake kuwaza (imagination) na kufurahia mchezo huo na mengineyo.

No comments:

Post a Comment