Mwanamke
huyo ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka alikuwa amevaa Blauzi
nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa silva, mnene kiasi,
mweusi na mwenye nywele ndefu.
Mwili
wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita Mchana baada ya
watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo
na kutoa taarifa Polisi.
Kwa
mujibu wa majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo, tukio hilo
linakisiwa kutokea usiku wa kuamkia jana huku baadhi ya kina mama
wakisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke akipiga mayowe katika eneo la
mnadani.
Naye
mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Mseven amesema
amepata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kufika katika eneo hilo
walibaini kuwa sehemu za siri za mwanamke huyo ziliingiziwa kitu chenye
ncha kali.
Jeshi
la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku
Mrakibu msaidizi wa Polisi Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika
katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.
MATUKIO KATIKA PICHA
MWENYEKITI WA MTAA NOEL MSEVEN AKIUFUNUA MWILI ILI WATU WAUONE.
MSEVEN AKIENDELEA KUWAONYESHA WATU MWILI HUO.
SAMAHANI KWA PICHA HIZI JAMANI,TUNAFANYA HIVI ILI WATU WAMTAMBUE MAANA HADI SASA HAJAPATA NDUGU.
HILI NDILO ENEO LA MAKABULI ALIPOKUTWA MAMA HUYO.
JESHI LA POLISI LIKIWA LIMEFIKA ENEO HILO KUUCHUKUA MWILI HUO.
WANANCHI WAKISAIDIANA NA POLISI KUUBEBA MWILI HUO.
MWILI UKIPELEKWA KUPAKIWA KWENYE GARI
MWILI UKIPAKAKIWA KWENYE GARI YA POLISI
KATIKA ENEO LA TUKIO MWILI UKIPAKIWA KATIKA GARI TAYARI KWA SAFARI YA MOCHWARI.
HILI NDILO KABULI LILIKOKUWA LIKICHIMBWA NA WATU WALIOUONA MWILI HUO.
MWILI UKIPELWA HOSPITALI
Source: Kijukuu blog
nouma xanaaaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeletehadi naogopa kulala