Pages

Saturday, August 24, 2013

Lulu Ameongea Haya Kuhusu Marekebisho Ya Filamu Ya Foolish Age, Na Kuhusu Uvumi Kuwa Imesimamishwa.

Kufuatia taarifa kuwa  Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeizuia filamu mpya ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ - Foolish Age, ambayo ilikuwa izinduliwe rasmi tarehe 30 mwezi huu kutokana na sababu za kimaadili, www.sammisago.com imeamua kulifuatilia swala hili ili kujua undani na ukweli wake.

 Kutokana uchunguzi wetu imefahamika kwa uhakika kuwa, Filamu hii haijasimamishwa ila imetakiwa kufanyiwa marekebisho baadhi ya sehemu ili kuiweka katika mahadhi na maadili yanayokubalika na jamii.
Taarifa zinaweka wazi kuwa, kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mitaa na mpaka sasa juhudi za kuifanyia marekebisho zimeshaanza ili ratiba za uzinduzi wake ziende kama ilivyopangwa.

Lulu Kaniambia " Filamu Haijafutwa Wala kusimamishwa, ila kuna baadhi ya vipande vinahitaji Marekebisho, Uzinduzi Upo kama kawaida"


No comments:

Post a Comment