Pages

Saturday, August 17, 2013

MTANZANIA ALIYEKAMATWA LOS ANGELES AKIRI KUINGIZA HEROINE MAREKANI


Mtu aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).

Shirika la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi. 
Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.


Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa laptop aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua.  Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu kuwasha komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama za kufunguliwa awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani ambapo walikuta gramu 800 za heroin zimefichwa. 
Mackubi alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa wamesema kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX wakisafirisha dawa za kulevya kwa njia hiyo.chanzo audiface jackson blog
Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11 Septemba

No comments:

Post a Comment