Mtu
aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela
nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya
heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).
Shirika
la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha
habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la
Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX
mjini Los Angeles akitokea Nairobi.
Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.
Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa laptop
aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua.
Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu
kuwasha komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama
za kufunguliwa awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa
ndani ambapo walikuta gramu 800 za heroin zimefichwa.
Mackubi alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni
Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa
wamesema kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX
wakisafirisha dawa za kulevya kwa njia hiyo.chanzo audiface jackson blog
Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11 Septemba
No comments:
Post a Comment