………………………………………………………………………………..
Kwa miaka 7 sasa TUSKER
PROJECT FAME imeendelea kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki
huku ikiwa na washiriki wengi kutoka Tanzania ambao hufanya vizuri
mashindano hayo. TUSKER PROJECT FAME imerudi tena kwa kishindo na mwaka
huu ikiwa ni msimu wa 6 wenye muonekano wa kipekee kwani
mashindano haya yameboreshwa na kupanua wigo wake ambapo washindi
katika usaili wataweza kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Tusker
project fame nchini Kenya.
Akiongea
na wana habari, Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Anitha
Msangi amesema “Tunawakaribisha watanzania wote ambao wanaamini
wanakipaji na wanaweza kudhihirisha kuwa kweli wao ni nyota katika
muziki. Ili waweze kujipatia nafasi ya kushiriki watanzania wanaweza
kuudhuria usaili utakaofanyika tarehe 7 na tarehe 8 Septemba katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Vigezo na masharti
vitazingatiwa na wanachotakiwa kufanya ni kuwapagawisha majaji na
kuwaonyesha kuwa kweli mshiriki anaweza kuipeperusha bendera ya Tanzania
katika mashindano”.
Mashindano
haya yatatikisa zaidi kwani Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro atakuwa
jaji katika mashindano haya. Yeye na majaji wenzake wataanza katika
usaili. Tanzania mwaka huu itapata nafasi ya kuwakilishwa na washiriki
wenye uwezo wa kujiamini kwa hali ya juu. Mashindano hayo yataoneshwa
katika televisheni inayoongoza kwa burudani Afrika Mashariki, East
Afrika Television (EATV)
“Najivunia
na najiona mwenye bahati kuwa miongoni mwa majaji watakaohakikisha
vipaji stahiki vinang`ara na kuiwakilisha nchi yetu. Kwangu hii ni fursa
kwa kuhakikisha vipaji vipya vinaendelea kuinuliwa na nawaahidi
watanzania kusimamia haki. Ninachokiomba kutoka kwa watanzania ni
kujiamini na kuonesha vipaji vyao kwani ukweli ni kwamba vipaji tunavyo
na tunaweza.” Alisema Zahiri Zorro.
Katika
mkutano huo na wanahabari miongoni mwa washiriki wa Tusker Project Fame
miaka ya nyuma alikuwepo, Aneth Kushaba. Alisisitiza suala la kujiamini
kama nguzo ya mafanikio katika kuhakikisha mshiriki anarudi na ushindi.
No comments:
Post a Comment