Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 17, 2013

TUSKER PROJECT FAME IMERUDI TENA!

  

1Meneja Masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa leo wakati wa uazinduzi wa Tuker Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010, Mwanamuziki Zahir Zoro na Meneja wa bia ya Tusker Lager Sia Shayo. 2Meneja wa bia ya Tusker Lager Sia Shayo akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa leo wakati wa uazinduzi wa Tuker Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010 na katikati ni  Mwanamuziki Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu . 3Mwanamuziki Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu  akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo kulia ni Janeth Kushaba mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka 2010.
………………………………………………………………………………..
Kwa miaka 7 sasa TUSKER PROJECT FAME imeendelea kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki huku ikiwa na washiriki wengi kutoka Tanzania ambao hufanya vizuri mashindano hayo. TUSKER PROJECT FAME imerudi tena kwa kishindo na mwaka huu ikiwa ni msimu wa 6 wenye muonekano wa kipekee kwani mashindano haya yameboreshwa na kupanua wigo wake ambapo washindi katika usaili wataweza kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Tusker project  fame  nchini Kenya.
Akiongea na wana habari, Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Anitha Msangi amesema “Tunawakaribisha watanzania wote ambao wanaamini wanakipaji na wanaweza kudhihirisha kuwa kweli wao ni nyota katika muziki. Ili waweze kujipatia nafasi ya kushiriki watanzania wanaweza kuudhuria usaili utakaofanyika tarehe 7 na tarehe 8 Septemba katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Vigezo na masharti vitazingatiwa na wanachotakiwa kufanya ni kuwapagawisha majaji na kuwaonyesha kuwa kweli mshiriki anaweza kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano”.
Mashindano haya yatatikisa zaidi kwani Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro atakuwa jaji katika mashindano haya.   Yeye na majaji wenzake  wataanza katika usaili. Tanzania mwaka huu itapata nafasi ya kuwakilishwa na washiriki wenye uwezo wa kujiamini kwa hali ya juu. Mashindano hayo yataoneshwa katika televisheni inayoongoza  kwa burudani Afrika Mashariki,  East Afrika Television (EATV)
“Najivunia na najiona mwenye bahati kuwa miongoni mwa majaji watakaohakikisha vipaji stahiki vinang`ara na kuiwakilisha nchi yetu. Kwangu hii ni fursa kwa kuhakikisha vipaji vipya vinaendelea kuinuliwa na nawaahidi watanzania kusimamia haki. Ninachokiomba kutoka kwa watanzania ni kujiamini na kuonesha vipaji vyao kwani ukweli ni kwamba vipaji tunavyo na tunaweza.” Alisema Zahiri Zorro.
Katika mkutano huo na wanahabari miongoni mwa washiriki wa Tusker Project Fame miaka ya nyuma alikuwepo, Aneth Kushaba. Alisisitiza suala la kujiamini kama nguzo ya mafanikio katika kuhakikisha mshiriki anarudi na ushindi.

No comments:

Post a Comment