ABIRIA WAKIWA WANASHUKA BAADA YA KUONA ASKARI HUYO WA USALAMA WA BARABARANI KUMVUTA DEREVA NA KUMALIZANA NAE PEMBENI
ASKARI
WA USALAMA WA BARABARANI AKIWA ANAPANDA KATIKA BASI BAADA YA ABIRIA
KUMJIA JUU NA KUDAI KUWA AMEKOSEA, HAPA ALILIWA ANATOA ABIRIA NA
KUWAPELEKA ENEO AMBAPO NDIPO MALIPO YASIYO HALALI YALIFANYIKA
ABIRIA
WAKIWA WANAENDELA KUMZONGA TRAFIKI HUYO AMBAYE ALIONEKANA ANAKIBURI NA
KULAZIMISHA DEREVA AENDE KITUONI KWA AJILI YA KULIPIA
KONDACTA WA BASI LA NEW FORCE WA KWANZA KUSHOTO AKIWASIHI ABIRIA WAINGIE NDANI YA GARI NA KWENDA KULIPIA
ABIRIA WAKIWA WANAPANDA KATIKA BASI TAYARI KWA KWENDA KULIPIA FINE ISIYO YA UHALALI NA UHALISIA
HAPA NDANI TRAFIKI HUYO AKIWA ANAWALAZIMISHA ABIRIA KUINGIA NDANI YA GARI ALI KUELEKEA KITUO KIDOGO KULIPIA.
MMOJA YA ABIRIA AKIJARIBU KUMUELEKEZA ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI JUU YA JAMBO HILO LAKINI ALIKUWA HAELEWI
HAPA ABIRIA WAKIWA WAMECHACHAMAA BAADA YA KUJIWA VIBAYA NA ASKARI HAO WA USALAMA WA BARABARANI.
HIZI NDIZO COPY ZA FAINI HIYO AMBAYO ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WALIKATAA KUTOA RISITI
HAPA ABIRIA WAKIWA WAMECHACHAMAA BAADA YA KUJIWA VIBAYA NA ASKARI HAO WA USALAMA WA BARABARANI.
HIZI NDIZO COPY ZA FAINI HIYO AMBAYO ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WALIKATAA KUTOA RISITI
*********
Katika
hari ya sinto fahamu leo majira saa tano na nusu maeneo ya Iringa
limetokea tukio la kusikitisha ambapo Askari wa usalama wa Barabarani
alilikamata Basi la abiria lililokuwa likitoka Mbeya kuelekea Dar es
salaam.
Trafiki
huyo aliyekamata Basi hilo lenye namba za usajili T111CLU kwa madai ya
kwamba kuna mtu ametoa taarifa ya kwamba aliovatekiwa kwa vurugu , na
kumtaka dereva alipe fine kwa kuwa kosa hilo ni uvunjifu wa sheria za
barabarani.
Hali
ilizidi kuwa tete zaidi baada ya askari huyo kuulizwa mtu aliye
ovatekiwa yuko wapi na kushindwa kumtaja huku abiria wakiwa
wamechachamaa kutaka kumjua kwa sababu mpaka wanakamatwa kulikuwa hakuna
hata sehemu ambapo Dereva huyo alicheza Rafu yoyote ile.
Baada
ya mzozo uliochukua takribani ya dakika tano huku abiria wakitaka
kumjua aliye toa taarifa hizo na Trafiki huyo kuto taka kumtaja kwa
madai ya kuwa mtu huyo hawezi kutajwa, aliamuru basi hilo lipelekwe
mpaka kituo kidogo ili liweze kutozwa faini.
Kitendo
hicho ambacho kilikuwa ni cha kionezi, kiliendelea na hali kuwa mbaya
zaidi baada ya ya Askari yule wa usalama wa Barabarani kutoa kauli na
kusema"Sasa wewe Dereva tumekukamata na upo na abiria wako hapa sasa
amua Moja unasikiliza Abiria wako au unalipa faini uendelee na safari?"
Na kuendelea kusema "abiria hawa wanashuka Dar es salaam wewe Utabaki
babarani" kauli hiyo ya kitisho iliwashangaza mashuhuda, huku Trafiki
mwengine pembeni akiwa ana wachimba mkwara waandishi wa habari waliofika
eneo lile na alisikika akisema "Hata kama ni waandishi hamuwezi kufanya
chochote" ilikuwa ni kauli ambayo yeye alizania ni ya Kitisho.
Baada
ya Hapo mmoja wa askari wa usalama wa barabarani alimwita Dereva pamoja
na Kondacta wake ili wapate kulipia pesa ambazo kimsingi hazikuwa na
TIJA yoyote ya kulipwa kwa sababu kulikuwa hakuna Ushahidi wa kutosha
kwamba ni kweli walikuwa wamefanya kosa na Abiria wote walikuwa
hawajaona kitendo hicho.
Baada
ya mzozo wa takribani dakika 10 Dereva aliamua kulipia Fine hiyo ya
kiasi cha Shilingi za Kitanzania 30,000 ambapo pia Dereva huyo alikili
kabisa kwamba risiti aliyopewa sio sahihi.
Hata
hivyo Madereva wa mabasi wamekuwa wakilalamika kila wakati ya kwamba
wamekuwa wakinyanyaswa sana kwamba wanapofika eneo la Ipogolo Trafiki
huwa wakiwasimamisha na kuambiwa kwamba wamechezea rafu magari madogo na
kulazimishwa kulipia faini wakati Gari husika ambalo limefanyiwa makosa
likiwa halipo, Wahusika wa mabasi wameongezea kwa kusema kwamba hakuna
uwiano wa kulipia faini hizo na kusema kwamba wanatakiwa kupewa risiti
ya Njano na wanapewa Risiti nyeupe.
Swali ni Je hali hii katika eneo la Iringa hasa pale Ipogoro itaendelea mpaka Lini? na je wahusika wanalizungumziaje hili?
Mpaka Abiria wanaondoka eneo la Tukio waliendelea kulaani kitendo kilicho tokea.
NA IRINGA YETU BLOG
NA IRINGA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment