Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, September 28, 2013

50 wauawa kwenye ghasia Sudan

130927090205 sudan 512x288 d nocredit 831fd

Maafisa wa usalama nchini Sudan wamewaua watu 50 katika maandamano yaliyofanywa kwa siku kadhaa kupinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo.
Polisi waliwatupia gesi ya kutoa machozi waandamanaji zaidi siku ya Ijumaa. 
Taarifa zinazohusianaSudan
Maafisa wanasema kuwa chini ya watu 29 wamefariki na kusema kuwa serikali ilikuwa haiwezi tena kumudu gharama ya ruzuku ya mafuta.
Waandamanaji wameikosoa serikali ya Rais Omar al-Bashir kwa hatua hii na kumtaka aondoke mamlakani.
Taasisi ya elimu ya maswala ya haki na amani pamoja na shirika la Amnesty International zimesema kuwa watu wamepata majeraha ya risasi kwenye vifua na vichwa kulingana na jamaa, madaktari na waandishi wa habari.
Kijana mwenye umri wa miaka 14 alikuwa miongoni mwa waathiriwa wengi waliokuwa kati ya umri wa miaka 19-26. Waliongeza kusema kuwa mamia ya watu wamezuiliwa.
"Kuwaua kwa kuwapiga risasi watu kwenye vifua na vichwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Sudan lazima isitishe ghasia hizi mara moja,'' alisema Lucy Freeman, Naibu mkurugenzi wa shirika la Amnesty International.
Duru za hospitalini zimeambia BBC kuwa takriban watu 60 wameuawa.
Maafis wa serikali ya Sudan bado hawajasema chochote kuhusu mauaji hayo lakini waziri wa habari Ahmed Belal Osman alisema kuwa idadi ya vifo ambayo ni juu zaidi ya watu 29 sio sawa.
Ghasia zilianza Jumatatu pale serikali ilipoondoa ruzuku kwa mafuta ili kupandisha ushuru. Hatua ya serikali kupunguza gharama ya matumizi ya pesa za umma, ilisababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kuwaathiri sana watu wa kipato cha chini

No comments:

Post a Comment