Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akizungumza na
wadau(hawapopichani) wanaohusika na sekta ya usafirishaji majini wakati
wa kongamano la kuadhimisha siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini
Mwanza hivi karibuni.
Naibu
Waziriwa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa sekta ya usafirishaji majini wakati wa kongamano la kuadhimisha
siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
TPA yaadhimisha siku ya Siku ya Bahari Duniani
Na Focus MaukiAfisa Mawasiliano-TPA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North.
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Bahari Duniani (IMO) linaadhimisha Siku ya Bahari Duniani, Septemba 26 kila mwaka.
Maadhimisho hayo hufanyika mara moja kila mwaka ambapo pamoja na mambo mengine Jumuiya ya Kimataifa ya Bahari ikiongozwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO), huyaadhimisha kwa kutathimini usimamiaji wa ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira baharini na katika maziwa.
Tanzania ikiwamo nchi nyingine wanachama wa IMO huadhimisha siku hii kwa kufanya maonyesho ya siku mbili ambayo huandaliwa na SUMATRA. Kwa mwaka huu maonyesho haya yamefanyika Septemba 25 na kufikia kilele chake Septemba 26 mwaka huu.
Pamoja na kuwa na maonyesho kwa umma, SUMATRA iliandaa kongamano lililofanyika Septemba 26 ambalo lililenga kuonyesha mchango wa Sekta ya Bahari na Bandari katika kukuza na kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.
Kaulimbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni, 'Maendeleo endelevu: Mchango wa IMO kupitia Agenda ya Rio +20'. Kwa mujibu wa SUMATRA kauli mbiu ya mwaka huu imechaguliwa kuonyesha mchango wa IMO kwa mwaka 2013 katika kubeba jukumu la kutekeleza makubaliano ya kimataifa juu ya kuleta maendeleo endelevu yaliyoafikiwa katika kikao kilichofanyika Juni 20 hadi 22, 2012, Rio de Janeiro, Brazil kijulikanacho kama 'Rio+20'.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Alhaj Ahmad Kilima amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Umoja wa Mataifa umechukua hatua za kimaendeleo kwa kuweka malengo mengi ili kufikia maendeleo endelevu ambayo hayatoathiri uwezo wa dunia, mfumo asilia pamoja na kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili jamii.
Sekta ya bahari ina mchango mkubwa katika mihimili mitatu ya maendeleo endelevu ambayo ni uchumi, jamii na utunzaji wa mazingira ya bahari. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha Bandari zake kote nchini, ili imeweka mazingira na miundombinu ya kisasa itakayotoa mchango katika kufikia malengo yaliyopo kitaifa na kimataifa.
-MWISHO-
No comments:
Post a Comment