Wanasema kwamba mwanafunzi akitoka na Zero shuleni hawezi kutimiza ndoto zake. Kwani uongo? Kala Jeremiah, mshindi wa tuzo tatu za mziki wa KILI anamalizia wimbo kwa kuwaasa vijana kwa kusema: PANDA MBEGU BORA, KITABU NDIYO MAISHA YAKO.
Wasanii walioimba wimbo huo ni: Linex, Roma, Linah, MwanaFA, Mwasiti, Stamina, Diamond, Maundo Zoro, Peter Msechu, Keisha na Kala Jeremiah.
Hebu gonga hapa uusikie wimbo huo:
http://bit.ly/12io5nU
Pia fuatilia mistari ya wimbo huo hapa chini:
Elimu bora ni muhimu kwa
kila mmoja wote tuelimike
tufikie malengo tokomeza ziro
kwa vitendo tokomeza ziro
Kiitikio: mwisho wa ziro x 8
Akakufundisha ukafika kuwa
mwalimu chonde chonde
moyo uliokuwa nao ualimu
wako kipindi kile ndicho
wanachohitaji wanafunzi
wako vilevile jiunge na sisi.
Nyerere alitupa chaki akaenda
kudai uhuru elimu urithi wa haki
acheni kupiga ndulu
Mama nishoneshee shati
Nakuahidi nitafaulu maticha wengi
mayanki kazeni wanangu wa Bwiru
Ongeza mishahara iwe motisha
zana za maabara na kukumbusha
okoa kizazi chetu ila
tokomeza ziro okey?
Wanafunzi shika nidhamu
isikuponyoke ni vabaya kukataa
elimu kwa vyovyote tambua
kwa nini uko shule kataa utoro
kataa utoro
Mwalimu fundisha ili mtoto
aelewe ipasavyo usifundishe
mtoto kudidimia kimawazo
maisha yanahitaji elimu
ndio msingi kwenye kila la muhimu
kama yatamshinda
hakuna zaidi yako wa kumlahumu
Elimu bora ni muhimu kwa
kila mmoja wote tuelimike
tufikie malengo tokomeza ziro
kwa vitendo tokomeza ziro
Kiitikio: mwisho wa ziro x 8
Ana ndoto kila mtoto haki
yake kuelimika aaaah
ni heshima ni lazima kila
mzazi kuwajibika aaah
tokomeza ziro kwenu
we ndo hero Baba Mama
wamaweka tumaini lao kwako
Kiongozi mzingo usiyethamini
elimu uliyesahau, ulifundishwa
ukapata vikakujenga tukakupa
nafasi utuongozee
Kila kitu kizuri duniani huletwa
na pesa elimu haina umri utasoma
hata MEMKWA fanya chaguo chagua
kitu kimoja Elimu ni ufunguo.
usipoteze uwekee holders
mitizamo hasi inafelisha vijana
ticha ingia class usitege
bila maana kuwa hero
uwe mshindi kila sekta
tokomeza Ziro usimchore
Messi NECTA.
Asiye na ndoto za urahis pia ama
kuwa msanii hujashangiliwa tena
msanii mkali uweze kufika mbali.
Sa vipi utapa na elimu unakataa
ooh vipi utapata na elimu unakataa.
Huku ukinyong’onyea kwa woga na
Kutojiamini ukikosa maarifa
na mbinu za kukutoa shimoni.
Kiitikio: Mwisho wa ziro, mwisho wa ziro x 8
Mazingira, mabaara, walimu wa
sayansi na hisabati pia, lishe
duni darasa chakavu lakini bado
we unaweza kujituma ukafanya vizuri
from Ziro to Hero. Ziro ni adui yetu
Kiitikio: mwisho wa ziro x 8
(Elimu bora ni muhimu kwa
kila mmoja wote tuelimike
tufikie malengo tokomeza ziro
kwa vitendo tokomeza ziro)
Panda mbegu bora kitabu ndio maisha yako
HAKIELIMU
No comments:
Post a Comment