Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akifungua warsha siku
tano kwa Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Mashariki
na Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika inayosisitiza umuhimu wa
ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli na majukumu ya Umoja wa Mataifa
katika za Kusini mwa Afrika yenye ujumbe wa Delivering As One (DAO)
kutoa matokeo ya pamoja katika kuratibisha na kuboresha majukumu ya
Umoja wa Mataifa katika nchini hizo.
Akifungua
warsha hiyo Dk. Kacou amesisitiza umuhimu wa mkutano kuwapa jukwaa
wafanyakazi wote wa Ofisi za waratibu wakazi jinsi ya kujielimisha na
kupata habari ya mabadiliko ya Dunia na majukumu ya Kikanda yanayoendana
na maboresho ya kuratibu shughuli za Umoja wa Mataifa wenye lengo la
kuleta matokeo ya pamoja.
Alisema
warsha hiyo itawajengea uwezo kwa washiriki umuhimu wa kujenga mazoea ya
kujielimisha kimkakati na stadi za kazi zenye kuleta ufanisi katika
kusaidia kuleta mabadiliko ya kazi za Umoja wa Mataifa katika nchi za
Kusini mwa Afrika.
Dk. Kacou
ameongeza katika kuleta matokeo ya pamoja Waratibu wakazi wanajukumu la
kuhakikisha Haki za Binadamu na Mashirika yanayotetea Haki za Binadamu
yanapewa wigo mpana katika kushiriki kwenye mchakato wa Demokrasia na
Haki za Binadamu.
Amefafanua
kuwa Mkutano huu unafanyika Tanzania kwa sababu ni nchi iliyoonyesha
mafanikio katika nyanja hizi za Kiuchumi, Kisiasa, Demokrasia na Haki za
Binadamu.
Warsha
hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Kikanda cha Maendeleo Umoja wa Mataifa
(UNDG) Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya
kuchukua na kupeleka mbele mabadiliko ya kimkakati yanayoleta matokeo ya
pamoja,chanzo:zainul mzige.
No comments:
Post a Comment