hdg
MAANDAMANO
ya wanahabari mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya
kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC) na mwandishi wa Chanel Ten Marehemu Daudi Mwangosi yatikisa
mji wa Iringa leo
Maandamano hayo ambayo yameanza majira ya saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yamepata kuzungukakatika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.
katika maeneo mbali mbali ambayo maandamano hayo yamepita likiwemo eneo la Uhindini , Mashine tatu, Soko kuu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani wananchi walilazimika kusitisha shughuli zao kushuhudia maandamano hayo ambayo yaliongozwa na askari wa usalama barabarani .

Akizungumza
baada ya kupokea maandamano hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw Leonard alisema
kuwa lengo la maandamano hayo ni kumkumbuka Mwangosi pamoja na kutazama
changamoto mbali mbali ambazo wanahabari wamekuwa wakikabiliana.
Alisema
kuwa hakuna mtanzania asiyetambua mchango wa Mwangosi katika uhai wake
na kuwa kutokana na mchango wake umoja wa vilabu vya waandishi wa habari
Tanzania (UTPC) umeanzisha tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa jina
la Daudi Mwangosi na mshindi atapewa kiasi cha Tsh milioni 10.
Alisema
tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka na UTPC na ili mwanahabari aweze
kushinda tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko suko katika kazi hiyo
,pia wale watakaopigania maslahi yao na fisa nyingine nyingi.
Hivyo
aliwataka wanahabari wanachama wa Vilabu vya wanahabari na wale wasio
wanachama ambao wanafanya kazi Tanzania kujitokeza kuchangamkia tuzo
hiyo.
Mbali hilo aliwataka wanahabari kuendelea kuzingatia maadili yao ya kazi hiyo ili kuongeza imani kwa watanzania .
Alisema kuwa iwapo wanahabari watafanya watazingatia maadili ya uandishi Taifa linaweza kupiga hatua katika maendeleo.
Wakati
huo huo IPC imetoa mikopo ya zaidi ya Tsh 500,000 kwa wanachama wake ili
kuwawezesha kuboresha zaidi shughuli zao kwa kununua vifaa vya kazi
Marehemu
Mwangosi aliuwawa na polisi septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha
Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa ufunguzi wa tawi la Chadema kijiji
cha Nyololo.
No comments:
Post a Comment