Pages

Tuesday, September 3, 2013

DK ALBERIC KACOU AFUNGUA WARSHA KWA WARATIBU

IMG 5252 131b6
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akifungua warsha siku tano kwa Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika inayosisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli na majukumu ya Umoja wa Mataifa katika za Kusini mwa Afrika yenye ujumbe wa Delivering As One (DAO) kutoa matokeo ya pamoja katika kuratibisha na kuboresha majukumu ya Umoja wa Mataifa katika nchini hizo.

Akifungua warsha hiyo Dk. Kacou amesisitiza umuhimu wa mkutano kuwapa jukwaa wafanyakazi wote wa Ofisi za waratibu wakazi jinsi ya kujielimisha na kupata habari ya mabadiliko ya Dunia na majukumu ya Kikanda yanayoendana na maboresho ya kuratibu shughuli za Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuleta matokeo ya pamoja.
Alisema warsha hiyo itawajengea uwezo kwa washiriki umuhimu wa kujenga mazoea ya kujielimisha kimkakati na stadi za kazi zenye kuleta ufanisi katika kusaidia kuleta mabadiliko ya kazi za Umoja wa Mataifa katika nchi za Kusini mwa Afrika.
Dk. Kacou ameongeza katika kuleta matokeo ya pamoja Waratibu wakazi wanajukumu la kuhakikisha Haki za Binadamu na Mashirika yanayotetea Haki za Binadamu yanapewa wigo mpana katika kushiriki kwenye mchakato wa Demokrasia na Haki za Binadamu.
Amefafanua kuwa Mkutano huu unafanyika Tanzania kwa sababu ni nchi iliyoonyesha mafanikio katika nyanja hizi za Kiuchumi, Kisiasa, Demokrasia na Haki za Binadamu.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Kikanda cha Maendeleo Umoja wa Mataifa (UNDG) Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya kuchukua na kupeleka mbele mabadiliko ya kimkakati yanayoleta matokeo ya pamoja,chanzo:zainul mzige.

No comments:

Post a Comment