Pages

Tuesday, September 3, 2013

MAANDAMANO YA KUMBUKUMBU YA MWANGOSI IRINGA

E84A0241 d368c
E84A0252 5001b
E84A0283 cb334
E84A0501 12885
E84A0510 cca21
E84A0536 1698e
E84A0542 6e7a7

hdg
MAANDAMANO ya wanahabari mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na mwandishi wa Chanel Ten Marehemu Daudi Mwangosi yatikisa mji wa Iringa leo
Maandamano hayo ambayo yameanza majira ya saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yamepata kuzungukakatika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.
katika maeneo mbali mbali ambayo maandamano hayo yamepita likiwemo eneo la Uhindini , Mashine tatu, Soko kuu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani wananchi walilazimika kusitisha shughuli zao kushuhudia maandamano hayo ambayo yaliongozwa na askari wa usalama barabarani .
Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw Leonard alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kumkumbuka Mwangosi pamoja na kutazama changamoto mbali mbali ambazo wanahabari wamekuwa wakikabiliana.

Alisema kuwa hakuna mtanzania asiyetambua mchango wa Mwangosi katika uhai wake na kuwa kutokana na mchango wake umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanzisha tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa jina la Daudi Mwangosi na mshindi atapewa kiasi cha Tsh milioni 10.

Alisema tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka na UTPC na ili mwanahabari aweze kushinda tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko suko katika kazi hiyo ,pia wale watakaopigania maslahi yao na fisa nyingine nyingi.

Hivyo aliwataka wanahabari wanachama wa Vilabu vya wanahabari na wale wasio wanachama ambao wanafanya kazi Tanzania kujitokeza kuchangamkia tuzo hiyo.

Mbali hilo aliwataka wanahabari kuendelea kuzingatia maadili yao ya kazi hiyo ili kuongeza imani kwa watanzania .

Alisema kuwa iwapo wanahabari watafanya watazingatia maadili ya uandishi Taifa linaweza kupiga hatua katika maendeleo.

Wakati huo huo IPC imetoa mikopo ya zaidi ya Tsh 500,000 kwa wanachama wake ili kuwawezesha kuboresha zaidi shughuli zao kwa kununua vifaa vya kazi

Marehemu Mwangosi aliuwawa na polisi septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa ufunguzi wa tawi la Chadema kijiji cha Nyololo.

No comments:

Post a Comment