SALAM MAALUM KUTOKA KWA LIBENEKE LA MICHUZI
Ankal
akipongezwa na blogger gwiji duniani kaka Ndesanjo Machas iku
alipoanzisha rasmi Globu ya Jamii katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia
jijini Helsinki, Finland, Septemba 8, 2005
Ankal na mai waifu wake na toto tundu Sellah wakikata keki kuadhimisha miaka 9 ya Globu ya Jamii usiku wa kuamkia leo
-----------------------------------------------------------
Ilikuwa siku ya
Alhamisi tarehe kama ya leo (Septemba 8,) miaka TISA iliyopita wakati Globu ya
Jamii ilipozaliwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki
Finland, kama utani tu. Kwa msemo mwingine, ni miaka TISA kamili leo toka Globu
ya Jamii ianze Libeneke la kuhabarisha wadau kwa mapicha na habari kemkem bila
kukosa hata siku moja
Kikosi kazi cha
Globu ya Jamii kingependa kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote duniani kote
kwa kampani mnayotupa kila saa, siku, wiki, miezi na hadi sasa ikiwa ni MIAKA
TISA kamili. Si jambo dogo, ukizingatia
katika safari hii njiani tumekutana na kila aina ya changamoto, kubwa kuliko
yote ikiwa ni kufanya kila tuwezalo kubakia hapa tulipo kwa kufuata weledi
pamoja na sera ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI, pamoja na kauli
mbiu kwa wadau watoa maoni ya kuwa waangalifu kutochafua hali ya hewa wala kujeruhi
hisia ya mtu wakati wa kutoa maoni.
Si rahisi
kumridhisha kila mdau, na kwa mujibu wa usemi wa Kimombo wa “What’s good for
the goose is bad for the hen” unaomaanisha hivyo. Yaani “Kilicho kizuri kwa
bata mzinga, ni kibaya kwa kuku”.
Katika kuadhimisha
hii MIAKA TISA ya Libeneke, Globu ya Jamii haitofanya sherehe ya pamoja na
wadau kama ilivyotarajiwa. Badala yake Ankal kajikakamua na kununua kajikeki na
kukata na kula na familia kwa niaba ya wadau. Ila ahadi yetu ni kwamba, panapo
majaaliwa, sherehe kubwa itaandaliwa mwakani wakati wa kuadhimisha MIAKA KUMI.
Ni mapema mno kusema itakuwaje, ila panapo uhai itakuwa SHEREHE KUBWA na inayostahili.
Kwanza
kabisa tunamshukuru Jalali Muumba wa vyote kwa tunu hii aliyoitupa.
Tunatambua kuwa tuna bahati ya sisi kuwa sisi, na kamwe bahati hiyo
uliyotupa, EWE MOLA, hatutoichezea...
Globu ya Jamii pia inachukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wake, ikiwa ni pamoja na VODACOM,
AIRTEL, UHURU ONE, TTCL, NMB, NBC, AZANIA
BANK, CRDB, NHC, PRECISION AIR, AIR UGANDA, NSSF, PSPF, DSTV, SKYLINK,
SERENGETI FREIGHT FORWADERS ‘WAZEE WA
KAZI’, SWIFT FREIGHT, GIRAFFE OCEAN VIW HOTEL, DR MKOMBOZI, na wengineo wote. Tunashukuru kwa kutuamini na
kuendelea kuendeleza nasi Libeneke.
Shukrani zingine za kipekee ziende kwa familia yangu kwa
uvumilivu wanaoonesha kwangu, pia kwa wadau kadhaa ambao tukiamua kuwataja wote
hapa itachukua ukurasa wote hu na tusiwe tumetaja japo robo yao. Kwa uchache tu,
na ambao ni kwa niaba ya wale ambao hatutotaja kwa ufinyu wa nafasi na pia
si kwa ubora wao, shukrani hizo
zimwendee kaka Ndesanjo Macha kwa kuwa wa kwanza kutufungulia na kutuongoza
njia na kutupa maudhui ambao baada ya kuyafuata, tumeona faida yake.
Washauri
wakuu wetu pia hatuwasahau katika hili. Nao ni Profesa Mark Mwandosya,
Mhe. January Makamba, Freddy Macha, Balozi Peter Kallaghe, Othman
Michuzi, Ahmad Michuzi, Christopher Makwaia MK, Steve Wassira jnr.,
Nathan Chiume, DJ Luke Joe wa Vijimambo, Waziri Ally, John Kitime, Alex
Perullo, Muhidin Maalim Gurumo, kaka Jeff Msangi, Boniface Makene, Kirk
Gills, Oscar Shelukindo, Ephraim Mafuru, Imani Kajula, Profesa Mbele,
Da' Chemi Chemponda, Ankal Beda Msimbe, kaka Assah Mwambene, Da' Tagie
Daisy Mwakawago, Shamim Zeze wa 8020 Fashions, Mama wa Mitindo Asia
Idarous na mumewe Mzee Khamsin, Ainde, kaka Asimwe Kabuga, Abdallah Ezza
na Fide Tungaraza wa Heslsinki na wengineo wengi tu. Ushauri wenu
tunauthamini na kuuheshimu!
Wengine ni viongozi
wote wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika, Naibu Spika na maofisa wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano pamoja
na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Viongozi maofisa wote wa vyama vya siasa, Viongozi wote
na watumishi wa taasisi za umma na
binafsi, Mablogger wote na mwisho ni wadau wote wanaotupa moyo kila kukicha. Asanteni
sana, sana, sana, sana. Hatuna cha
kuwapa zaidi ya hizo SHUKURANI kutoka katika kilindi cha moyo wetu. MOLA AWE
NANYI, NA AWAZIDISHIE PALE PALIPOPUNGUA.
Hatuna la zaidi la
kusema zaidi ya kuahidi kwamba tutaendeleza Libeneke kwa moyo wetu wote huku
tukipiga magoti kuwaomba wapendwa wadau wetu duniani kote muendelee kutupa
kampani, kwani bila ninyi sisi si lolote si chochote. Pia tunaomba radhi pale
tunapoteleza kama binaadamu yeyote ambaye daima duni si mkamilifu, ambapo
likitokea litalotokea si kwa makusudi ama nia mbaya bali ni kwa udhaifu huo huo
wa kibinaadamu.
Naomba kuwasilisha,
Wenu Mnyenyekevu,
Muhidin Issa
Michuzi “Ankal”
DJ SEK BLOG INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA ANKALI KWA KUTIMIZA MIAKA 9 KATIKA KUBLOGISHA,NA KUWA MFANO WA KUIGWA.MUNGU AENDELEE KUKUPA UZIMA NA ABARIKI KAZI YA MIKONO YAKO
No comments:
Post a Comment