Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 2, 2013

KOCHA MSAIDIZI ABWAGA MANYANGA YANGA, KISA KUTOTHAMINIWA KIASI CHA KULAZWA CHINI KAMBINI

Ameng'atuka; Abubakar Salum 'Sure Boy'

Na Prince Akbar,
KOCHA Msaidizi wa timu ya pili ya Yanga SC, maarufu kama Yanga B, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ ameacha kazi katika timu hiyo kwa sababu moja kubwa; kutothaminiwa.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga SC, zimesema kwamba winga huyo hodari wa zamani wa wana Jangwani hao ameamua kuacha kazi kwa sababu za kimaslahi.
Imeelezwa Sure Boy Sr. hakuwa anaridhika na kiasi cha Sh. 200,000 alichokuwa analipwa kwa mwezi licha ya kuamini amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuibua vipaji vya vijana ambao baadhi yao wamepandishwa timu A msimu huu.
Pamoja na hayo, baba huyo wa kiungo wa Azam FC, na timu ya taifa, Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ inaelezwa alikerwa zaidi timu B ilipokwenda Zanzibar katika michezo ya Pasaka, akalazwa chini.
Imeelezwa timu iliporudi kutoka Zanzibar ndipo naye akaacha kazi. Alipotafutwa Sure Boy mwenyewe kuzungumzia suala hilo alisema; “Nimeacha kazi, sipo Yanga. Basi. Kazi ni hiari ya mtu, akiridhika na maslahi anafanya, kama vipi anaacha,”alisema.
Da! Baba kaacha kazi; Salum Abubakar 'Sure Boy Jr.' baba yake kaacha kazi Yanga SC 
   

Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako aliyecheza na Sure Boy Sr. enzi zake katika timu hiyo, hakupatikana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo.

No comments:

Post a Comment