Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 2, 2013

Tusker Project Fame 6 YAENDELEA KUSAKA VIPAJI MIKOANI

PICHA ZINAONESHA MATUKIO MBALIMBALI YA BURUDANI NA WASHIRIKI WALIOJITOKEZA KATIKA MIKOA HIYO.
 
28th - 31th 2013 mkoani Arusha, Mbeya, Mwanza na tarehe 1 septemba shangwe hizo zilihamia jijini Dar es salaam.  

Kufuatia usahili utakaofanyika hivi karibuni wa nani ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kusaka kipaji bora cha kuimba Afrika Mashariki ambao unategemewa kufanyika tarehe 7 na 8 mwezi huu, kampuni ya bia ya Serengeti imewaburudisha watanzania wa mikoni na kuwapa fursa ya kushiriki usahili huo kwa kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuimba na mshindi kujipatia tiketi ya kusafiri mpaka Dar es salaam ili kushiriki katika usahili huo.

 Wateja wa kampuni hiyo mkoani Arusha walijipatia tisheti, bia za bure na washindi wa kipaji cha kuimba walipata tiketi za bure za kushiriki usaili  mkoani Dar es salaam. washindi hao ni pamoja na David Jamal,Bartazal Kauki na wengine wengi. pia mkoani mbeya mashindano hayo yalifanyika katika baa za Rombo Bar, Mama Land Bar na Airport Bar ambapo kila bar ilitoa mshindi na kujipatia tiketi ya kushiriki usaili.

No comments:

Post a Comment