skip to main |
skip to sidebar
MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA TAMASHA LA 11 LA TGNP JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA
Tamasha la 11 la mtandao wa jinsia
Tanzania (TGNP) limeanza kwa maandamano katika ofisi za TGNP eneo la
Mabibo jijini Dar es Salaam.
Maandamano hayo yameanzia lango kuu la ofisi za TGNP na kuhitimishwa katika viwanja vya tamasha eneo hilo la TGNP.
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha
hilo mkurugenzi wa TGNP Usu Mallya alisema wakati TGNP inaazimisha
tamasha hilo bado inajivunia mapambano makubwa yaliyodumu kwa miaka 16
katika kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi
wanaposhinda kesi hiyo.
Hivyo alisema ushindi wa kesi hiyo
dhidi ya jengo hilo utawafanya sasa kuendelea kuboresha zaidi jengop
hilo na kulifanya kuwa la kisasa zaidi na kuendeleza mafunzo mbali
mbali.
Chanzo:Francisgodwinblog
No comments:
Post a Comment