Na Amina Abeid (ZJMMC) 3/9/2013.
Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Davis Adolf
Mwamunyange leo amewatunuku Nishani Maafisa na Askari 39 wa JWTZ katika
hafla iliyofanyika Kambi ya Jeshi ya Bavuai nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
Mwamunyange
amefanya zoezi hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kufanya Idadi
ya Wanajeshi waliotunikiwa Nishani msimu huu kutimia 939 Tanzania kwa
ujumla.
hdg
Zoezi
hilo limefanyika kwa Maafisa na Askari Jeshi wenye sifa za kulitumikia
Jeshi kwa muda mrefu na kwa tabia ya kuweza kusifika katika Jeshi hilo.
Katika
Zoezi hilo Maafisa wawili walitunikiwa Nishani ya Utumishi uliotukuka,
Maafisa sita Wametunukiwa Nishani ya muda mrefu ambapo Askari 31
wametunukiwa nishani ya tabia njema.
Akifafanua
kuhusu Nishani hizo Mwamunyange amesema Nishani ya Utumishi uliotukuka
hutolewa kwa Maafisa wenye cheo cha Meja kwenda juu ambao wametumikia
Jeshi kwa miaka isiopungua 20 mfululizo.
Amesema
Nishani ya Utumishi mrefu hutolewa kwa Maafisa na Askari wa JWTZ ambao
wametimiza utumishi usiopungua miaka 15 mfululizo na nishani ya Utumishi
mrefu na tabia njema huvishwa Askari wa JWTZ waliotumikia Jeshi
mfululizo kwa muda usiopungua miaka 15.
Mkuu huyo
wa Jeshi amesema Utaratibu huo wa kutunuku nishani umekuwa ukifanywa
kwa muda mrefu kwa lengo la kupata Viongozi na Makamanda bora wa Jeshi
ambao wametumikia Taifa lao kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu.
Kwa
upande wake mmoja wa Watunukiwa wa Nishani ya Utumishi wa Muda mrefu na
tabia njema Saida Said amesema, amefarajika kupata nishani hiyo kwani
itamtambulisha Jeshini kuwa ana tabia njema.
Zoezi la
kutunuku nishani kwa Maafisa na Askari wa JWTZ limefanyika katika kituo
cha KJ 12,Zanzibar na linatarajiwa kuendelea kwa vituo vingine nchi
Nzima.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR-03/09/2013
No comments:
Post a Comment