Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 12, 2013

MAZUNGUMZO YA TIMU YA SUNDERLAND NA WIZARA YA MALIASILI NA UTAMADUNI.

Picha za matukio ya michezo.

Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson (wa pili kutoka kulia) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam  juu mazungumzo ya awali ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki(wa pili kutoka kushoto) na Mwakilishi wa timu ya Sunderland hapa nchini Edmund Hazzal (kulia).


Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) leo jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki.


Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson (kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (KUSHOTO),mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo.


Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson (kulia) akiongea na waandishi wa habari hapo pichani jana jijini Dar es salaam  juu ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Dar es salaam  juu ya mazungumzo ya awali kati ya timu ya Sunderland ya Uingereza ya kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto).


(Picha zote na Idara ya Habari Maelezo)

No comments:

Post a Comment