WATUHUMIWA watatu kati ya watano
waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa fedha kwenye
Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
wamehukumiwa kifungo jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kuwatia hatiani ambapo kati yao ni mke na mume.
Mke na mue hao ni Manase Makale
aliyetupwa jela miaka 5 na mkewe Eddah Makale aliyetupa jela miezi 18
sawa na mwaka mmoja na nusu Pamoja na Bahati Mahenge, aliyehukumiwa
kifungo cha Miaka 7 lupango.
Mbali na hukumu hiyo washitakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh1.86 bilioni za EPA, katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kupitia Kampuni ya Changanyikeni
Residential Complex wametakiwa kulipa fedha kiasi cha Sh 1.5 Bilioni.
Washitakiwa wawili wameachiwa huru na Mahakama hiyo baada ya Mahakama kushindwa kuwatia hatiani.
CHANZO FATHER KIDEVU BLOG
No comments:
Post a Comment