Pages

Thursday, September 5, 2013

Moto Waadhiri Nyumba ya Wanafunzi wa Al Rahamyn iliopo Mpendae Zanzibar


Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa katika zoezi ya kuuzima moto uliokuwa ukiwaka katika Nyumba ya Dahaliya ya Wanawake ya Al Haraymn Mpendae baada ya kutokea hitilafu ya umeme na kuteketeza karibu malizote za Wanafunzi wanaoishi katika Nyumba hiyo leo mchana, katika ajali hiyo hakuna Mwanafunzi aliyejeruhiwa katika moto huo.
Akasi wa Kikosi cha Zimamoto wakiwa katika jitihada za kuuzima moto uliokuwa ukiwaka katika Nyumba ya Dahaliya ya Wanawake ya Skuli ya Al Rahamny Mpendae leo.mchana Chanzo cha moto huo hakijajulikana.zaidi ya mali za shilingi milioni 100 zimeteketea ikiwemo nyumba yenyewe kuharibika vibara kutokana na moto huo.
   
Wananchi wakiwa eneo la tukio katika mitaa ya Mpendae kwa mchina wakati nyumba hiyo ikiwa moto.
Askari wa Zima moto wakiwa katika zoezi hilo la kuzima moto huo.


Hivi ndivyoilivyoharibika nyumba hiyo baada ya kuungua kwa moto chanzo chake hakijajulikana, na hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto.

Mmmoja wa Mwanafunzi aliyekuwema katika dahaliya hiyo wakati ikiwa moto na kuwahi kutolewa akiwa amelala akisaidiwa na Mwalimu wa Skuli hiyo, Dahaliya hiyo inakadiriwa kuwa na Wanafunzi 25 wa Skuli ya Al Haramyn wanaishi, wakati wa tukio baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha na huku moto unawaka na kuokolewa na Wananchi na Walimu wa skuli hiyo waliowahi kutowa msaada kabla ya kufika kwa Kikosi cha Zimamoto na kuendelea kuuzima moto huo.

  

Afisa wa Kikosi cha Zimamota Zanzibar akizungumza na waanddishi wa habari waliofika eneo la tukio wakati wa zoezi la kuzima moto huo, leo mchana na kusema kikosi chake kimearifiwa tukio mnamo saa 11.45 na kuwahi eneo la tukio.

Mfanyakazi wa Skuli hiyo akizungumza na Waanddishi wa habari kutokana na tukio hilo la moto lililoikumba moja ya jengo la kuishi wanafunzi wa skuli hiyo.  (Picha kwa hisani ya ZanziNews)

Al Rahamyn Zanzibar 

No comments:

Post a Comment