Pages

Saturday, September 28, 2013

MSANII DULLY SYKES ATANGAZA KUUZA STUDIO YAKE


Msanii Dully Sykes ametangaza kuwa anauza studio yake ya Dhahabu Rec iliyoko Tabata kwasababu anataka kubaki na studio moja ambayo ni 4.12.Dully alisema kuwa kwa yeyote ambaye atajitokeza kununua studio hiyo atamuuzia vifaa vilivyopo ndani pamoja na jina la Dhahabu Rec.Kwa yeyote anayetaka kununua studio hiyo amtafute.
Wakati huo huo msanii huyo ambaye yupo kwenye orodha ya wasanii wenye nyimbo 'hits' nyingi hapa Tanzania,kwa mujibu wake mwenyewe 56,alisema kuwa tangu aanze muziki mpaka leo hajawahi kutumia hela yake ya mfukoni kulipia wimbo wowote studio.Dully pia anasema anatarajia kuachia wimbo wake mpya wiki ijayo unaoenda kwa jina la 'Kabinti Special' wimbo ambao anasema ameufanya kwaajili ya mashabiki wake wa kike,”video iko tayari,siku itakapofika ntaachia wimbo na video hiyo ambayo anaamini ina ubora wa hali ya juu”, Dully.CHANZO ANNA PETER

No comments:

Post a Comment