Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya
bilionea wa madini Erasto Msuya,Sharifu Mohamed na Musa
Mangu wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya
wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya
wakiwa mahakamani.
Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro
na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi
hiyo.
Mtuhumiwa Sharifu Mohamed
akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa
kesi hiyo .
Dada wa marehemu Msuya
aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya
kuahirishwa kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya
aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya
kuahirishwa kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya
aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu
mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
Mdogo wa marehemu Msuya
aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari
mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mdogo wa marehemu Msuya
aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari
mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mama mzazi wa marehemu Erasto
akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la
familia.
Umati mkubwa wa wananchi
ulifurika mahakamani hapo
Ndugu
wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti
7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji
wa kesi hiyo.
Ndugu hao ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote walipoteza fahamu.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.
Wakili wa Serikali Stella
Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.
Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi.
Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.
Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.
Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.
Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.
No comments:
Post a Comment