Wafanyakazi wakionesha mabango yaliyobeba ujumbe wao.
Wafanyakazi wakiongea na waandishi.
Mkuu wa mkoa akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika eneo hilo.
Geti kubwa la kuingia kwenye kampuni hiyo likiwa limefungwa.
Wafanyakazi wa kampuni iliyokula tenda ya kutengeneza barabara za mabasi yaendayo kasi jijini Dar, wamejikuta wakiingia kwenye mgomo wakishinikiza walipwe madai yao ya muda mrefu na kuongezewa mishahara yao.
Tukio hilo limetokea leo mchana, makao makuu ya kampuni hiyo maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam ambapo mamia ya wafanyakazi waliandamana kwa kugomea kufanya kazi hali iliyomlazimu Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadick kuingilia kati suala hilo.
Wakizungumza katika nyakati tofauti, wafanyakazi hao walisema kuwa, wamekuwa wakidai malimbikizi ya stahiki zao kwa muda mrefu bila matekelezo yoyote huku wengi walilalamikia kitendo cha kampuni hiyo kutoa ajira kwa wahindi wanaolipwa mishahara mikubwa na kuwaacha wazawa ambao wanalipwa mishahara midogo au kubakia wakisota kwenye vibarua bila kuajiriwa.
Hata hivyo baada ya kikao cha muda mrefu kati ya viongozi wa kampuni hiyo na Mkuu wa Mkoa, walikubaliana kuwalipa wafanyakazi stahiki zote na kupandisha viwango cha mishahara yao kuendana na kanuni za ajira, ndani ya siku kumi kuanzia hii leo.
Hadi kamera zetu zinaondoka eneo la tukio kulikuwa hakuna maelewano kati ya wafanyakazi na viongozi wa kampuni hiyo kwa kile kilichobainika kuwa hawakuwa na imani nao.
(Picha na Chande Abdallah / GPL)
No comments:
Post a Comment