Watanzania
tumezoea kuburuzwa kwa upepo, na safari hii, Waziri wa Uchukuzi
Harrison Mwakyembe, amekua akifanya atakavyo bila kuhojiwa kutokana na
Watanzania kuzolewa na upepo wa mbwembwe zake bila kuhoji chochote.
Ni Waziri
Mwakyembe ambaye aliishinikiza Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA)
kumtimua Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraem Mgawe na kumleta
Madeni Kipande, lakini jana kwa mshangao ndiye ameiambia bodi ya sasa
kwamba haina mamlaka ya kumtimua Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa TPA na Kaimu
Mkurugenzi wa IT, Mjumbe wa NEC bwana Magesa. Anasema sheria na kanuni
haziipi mamlaka hayo bodi. Sasa Mgawe sheria ziliipa bodi mamlaka na leo
sheria hiyo hiyo (akiwa Mwanasheria) haina mamlaka na hakujawahi
kufanyika marekebisho yoyote.
Kwanza
baada ya kikao cha Bodi cha Jumamosi kuibua hoja 22 za kumuondoa DG
Kipande, kikao kikapanga kuendelea jana Jumapili katika hoteli ya
Southern Sun lakini ghafla wajumbe wakaambiwa kimehamishiwa TPA
Boardroom lakini Mwakyembe akakutana na Kipande na Mwenyekiti wa Bodi
Southern Sun kabla ya kuja TPA na kuwafokea wajumbe wa bodi na kufunga
kikao huku akiagiza kikao kijacho Bodi imfuate Dodoma watakapofanya
kikao kingine. Kati ya wajumbe wanane wanne walitaka kuachia ngazi jana
hiyo lakini busara ikatumika kuwambia wasubiri waone kitakachotokea.
Kibaya zaidi ni Mwakyembe kuwatisha wajumbe kwamba ameongea na Rais
Kikwete huko aliko na amempa nguvu ya kuwazuia Bodi wasifanye maamuzi
yoyote, jambo ambalo limeelezwa kutia shaka kama kweli JK ametoa maagizo
hayo akiwa nje wakati kuna Makamu na Waziri Mkuu wako nchini na halikua
jambo la dharura.
Kama
tunavyokumbuka Mwakyembe alikataa kufanya kazi na bodi ya zamani 7bu
ilipingana naye katika taratibu nzima alizotumia za kulazimisha Bodi
wausimamishe uongozi wote wa juu wa Bandari wakati huo . Siku hiyo
alipolazimisha Bodi almanusra wajumbe wote wajiuzulu mbele yake ikabidi
baadhi yao watumie busara kusitisha kujiuzulu huko
Ni
Mwakyembe aliyeunda Kamati ya kuchunguza TPA ikilipwa fedha na TPA na
kamati hiyo Mwenyekiti alilipwa 930,000 kwa siku, wajumbe 7+1 katibu
kila mmoja 630,000 kwa siku na walilala na kupata huduma zote Hoteli
Sourthen Sun USD 200 kwa siku (kulala tu) na walikaa kwa zaidi ya siku
60 na kuomba kuongezewa zaidi. Hadi leo ripoti ni siri maana imejaa
majungu.
No comments:
Post a Comment