Kwa mara ya kwanza katika historia ya mji wa Kahama na vitongoji vyake, wakazi wake walipata nafasi ya kuwashuhudia wakali wa muziki zaidi ya 10 katika jukwaa moja katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 lililofanyika katika uwanja wa taiga Kahama na kushuhudiwa na maelfu ya wakazi wa rika zote waliojitokeza na kuujaza uwanja wote. Wakali hao Linex, Profesa Jay, Roma, Ben Pol, Fid. Q, Lady Jaydee, Izzo Bizness, Barnaba na Recho walilishambulia jukwaa kwa masaa sita mfululizo huku wakati mmoja wakipata nafasi ya kumuimbia Ben Pol wimbo wa Birthday kutokana na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa usiku wa kuamkia Jumapili.
Recho na madansa wake katika steji ya Kili Music Tour Kahama
Shabiki mmoja alipata nafasi ya kucheza na Rech
Kutoka backstage: Izzo Bizness, Alice, Fid Q, Kala Jeremiah na Ben Pol
Ben Pol na Alice wakiimba wimbo wao mpya wa Waubani
Barnaba Boy jukwaani
Izzo Bishara, Izzo Bizness akiiwakilisha Mbeya mjini Kahama
Hip Hop ikiendelea kuwakilishwa na Kala Jeremiah
Kala Jeremiah akiwauliza mashabiki kama wameilewa Kikwetu kwetu
Roma Mkatoliki akiwarusha mashabiki waliofurika uwanja wa taifa Kahama
Ma-DJ kazini kuhakikisha hakuna kinachoharibika
Linex akiwa na wadau Shaaban Mpondela na Pius toka Frontline Novelli
Lady Jaydee na Profesa Jay wakiimba Joto Hasira
No comments:
Post a Comment