Pages

Friday, September 6, 2013

Tazama Picha::MSIKITI WATEKETEA KWA MOTO MJINI DODOMA......MOTO WA JIKO WADAIWA KUWA CHANZO...!!



Msikiti mkubwa wa Answar Sunna  uliopo  barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika....

Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mpekuzi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo...

Hata  hivyo, shuhuda  mwingine  aliyeongea  na  mtandao  huu  amedai    kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  hitilafu  ya  umeme  iliyoanzia  ghorofa  ya  juu  ya  jengo  hilo.
 
Kwa  mujibu  wa  mashuhuda  hao, moto  huo  umefanikiwa  kudhibitiwa  na  jeshi  la  zima  moto  na  kwamba  hakuna  mtu  aliyepoteza  maisha  kutokana  na  moto  huo.

Tunaendelea  kufuatilia  undani  wa  tukio  hili.

No comments:

Post a Comment