Mdau wa Kilimo kutoka mkoani
Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa zinazopatikana kwenye
kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa
mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la kilimo.
Sehemu ya vijana waliojitokeza k wa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana
Muwakilishi
wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana
mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika
mapema leo kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
Mmoja
wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto
Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake
waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia
fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
Baadhi
ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi
kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni
ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya
(hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,f
iliofanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
Mkali
wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya
wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo
iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya
kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo
Kisanji kilichopoo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni
ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza jambo na msanii wa
muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa Pili ndani ya semina ya Fursa kwa
vijana.
Muwakilishi kutoka shirika la
TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo ya fursa kwa vijana
na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.na LUKAZA BLOG
No comments:
Post a Comment