WILAYA YA RUNGWE - WATUHUMIWA 34 WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 25.09.2013 NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KULA NJAMA NA KUFANYA FUJO/KUFUNGA BARABARA KUU MBEYA/TUKUYU KWA MAWE NA MAGOGO.
§ MNAMO
TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:35HRS HUKO KATIKA MAHAKAMA
YA WILAYAILIYOPO - TUKUYU MJINI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA
MBEYA. LAURENT S/O NICHOLAUS KASWAGA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA
KIJIJI CHA IBURA – KIWIRANA WENZAKE 33 WALIFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA
YA WILAYA NA KUSOMEWA MASHTAKA MAWILI 1. KULA NJAMA NA 2. KUFANYA FUJO.
AIDHA WATUHUMIWA WALISOMEWA MASHTAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA
POLISI F.3644 D/C JOEL MBELE YA HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO MHE. MEBO
MALAKASUKA.
§ KATIKA
SHAURI HILO LA JINAI NO. 169/2013 WASHTAKIWA WOTE WAMEPELEKWA GEREZANI
AMBAPO UAMUZI WA KUPEWA AU KUTOPEWA DHAMANA UTATOLEWA NA
MAHAKAMA TAREHE 09.10.2013.
§ AWALI MNAMO
TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI YA SAA 18:00HRS HADI SAA 22:00HRS HUKO
KATIKA KATA YA KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA –
KATI NAKARASHA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI
YASIPITE NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA
HIYO. THAMANI HALISI YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO KUFAHAMIKA.
§ HATA
HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA TOYOTA
L/CRUISER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI
YA MAREHEMU WATATULILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA
WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA TOYOTA COASTER NA
KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI NA UHARIBIFU KWA MAGARI YOTE
MAWILI. CHANZO CHA VURUGU HIZO NI MADAI YA KUONGEZEWA USHURU WA MAZAO
[NDIZI] KUTOKA TSHS 100/= ULIOANZA KUTUMIKA MWAKA 1989 NA KUFIKIA TSHS
200/= WAKISHINIKIZA URUDISHWE USHURU WA ZAMANI NA KUFUATIA VURUGU HIZO
JUMLA YA WATUHUMIWA 43WALIKAMATWA.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA CHANGAMOTO KATIKA JAMII HAZIWEZI
KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE
UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO KERO NA MAONI YAO KATIKA MAMLAKA
HUSIKA NA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI KWA KUZINGATIA
HOJA.
AIDHA
ANASISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI
WENGINE WA BARABARA WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA
MBALIMBALI PIA KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE
NA KWAMBA JESHI LA POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA
KISHERIA WATU /KIKUNDI CHA WATU WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI.KWA
SASA HALI YA ENEO HILO NI |
No comments:
Post a Comment