Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 3, 2013

USAJILI WA FABIO COENTRAO KWENDA MANCHESTER UNITED WAINGIA ZENGWE DAKIKA YA MWISHO YA USAJILI - HATMA YAKE KUJULIKANA LEO

Usajili wa mkopo wa beki wa kushoto wa Real MadridFabio Coentrao kwenda Manchester United umeingia dosari wakati klabu hiyo ya England ikusubiri kujua kwamba nyaraka muhimu zilifika kwa wakati ili dili hilo kutibitishwa.

Wakiwa wamemkosa Leighton Baines, meneja wa Red Devils  David Moyes alimgeukia Coentrao na inaonekana walijitahidi kufanya kila wawezalo kufanikisha usajili huo ambao mwanzoni ulithibitishwa na maofisa wa La Liga.

Jana usiku saa 10.45pm kwa saa za Spain, La Liga ilitangaza dili la Coentrao na usajili mwingine wa Real Madrid kumchukua kwa mkopo beki wa kibrazil Guilherme Siqueira kutoka Granada.

Lakini taarifa zote hizi mbili baadae ziliondolewa, huku ripoti nchini Hispania zikisema kwamba Benfica walizidi mbio Real kwa  Siqueira, matokeo yake Real wakasitisha usajili wa mkopo wa  Coentrao katika dakika ya mwisho.

United tayari wameshathibitisha usajili wa Marouane Fellaini katika mtandao wao na wanatarajia kutoa taarifa rasmi kuhusiana na Coentrao mapema LEO ASUBUHI baada ya kujua hatma ya dili lao.

No comments:

Post a Comment