Vurugu
kubwa zilizotokea Bungeni muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa
wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya
Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe.
Freeman Mbowe.
****
Vurugu
kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri
ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe
ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.
Chanzo
cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe
kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa
kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa
mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala
huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani
ulishapita kwenye hatua mbalimbali.
Mara
baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai
aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema
achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga
uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni
wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya
mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
No comments:
Post a Comment