Kundi linaloongozwa na Ake Sellstorm lilikwenda nchi jirani ya Lebanon jumatano na kusafiri kwa kutumia gari hadi Damascus.
Kwanza walikwenda Syria mwezi uliopita kufanya uchunguzi wa mashambulizi matatu ikiwemo lile la mwezi Machi nje ya mji wa Aleppo ambalo serikali ya Syria na wapiganaji waasi wanashutumiana.
Kundi hilo lilihamisha mwelekeo wake wa ujumbe wa wiki mbili na kuzingatia shambulizi jipya nje ya Damascus ambako waligundua kwamba silaha za kemikali zilitumika.
Wakati huohuo Jumatano kundi la waasi 13 lilitoa taarifa ya pamoja kupinga baraza la upinzani la taifa la Syria likisema kuwa haliwakilishi tena ushawishi wao.
Watu wengi waliokimbia nchi hiyo wamekwenda nchi jirani ikiwemo Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment