Naibu
Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos Makala akizungumza
na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya
Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.Mkurugenzi
wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi kuhusu Maonyesho ya Wiki ya
Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na
kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kujiletea maendeleo.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiwa
ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma
wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka Zanzibar
wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiangalia
gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya asili na mbunifu
Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari hilo ambalo limekua
kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia katika shughuli zake
za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 180 kwa saa.Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiingia ndani ya gari hilo.Sehemu
ya mbele ya gari hilo ambalo limewavutia vijana wengi wakati wa
maonyesho ya wiki ya vijana mkoani Iringa kama inavyoonekana huku
mbunifu wa gari hilo Bw. Keny Joseph (kushoto) akirekebisha baadhi ya
vitu katika gari lake.Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akipata
maelezo kuhusu mifumo ya kompyuta katika banda la VETA mkoa wa Iringa
wakati wa Maonyesho ya wiki ya Vijana kitaifa yanayofanyika katika
viwanja vya Mlandege manispaa ya Iringa.Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma (kulia) na Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi wakitazama na kuonyesha
kuvutiwa na baadhi ya bidhaa zilizokuwa katika banda la maonyesho la
Vijana wa mkoa wa Dar es salaam.Mkurugenzi
Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Wanawake kutoka
Zanzibar Bw.Mohamed Salim Alli akifungua mdahalo wa Vijana wakati wa
Wiki ya Vijana katika Ukumbi wa VETA mkoani IringaVijana
wakishiriki mdahalo wa wazi wa Wiki ya Vijana , Kumbukumbu ya Mwalimu
Julius Nyerere , Mbio za Mwenge wa Uhuru na Fursa za uwekezaji
zinazopatikana katika mkoa wa Iringa leo katika ukumbi wa VETA Iringa.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
No comments:
Post a Comment