Pages

Wednesday, October 16, 2013

ANGALIA PICHA MAMA YAKE UFOO SARO ALIVYOAGWA JANA


 Mamia ya wakazi wa Kibaha mkoani pwani pamoja na jiji la Dar es Salaam walimiminika kwa wingi nyumbani kwa Marehemu Anastazia Saro Kibamba Kibwegere kutoa heshima za mwisho kwa mama wa Mwanahabari Ufoo Saro aliye uwawa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenza wa binti yake huyo ambaye pia alijeruhiwa kwa risasi. 
Kwa mujibu wa ripoti ya madkatari walioufanyia uvchunguzi mwili wa Marehemu, Muuaji ambaye alitambulika kwa jina la Anthery Mushi ambaye nae alijiua baada ya kutekeleza tukio hilo alimpiga risasi tano. 
 Mwili wa marehemu ukiwa nyumbani kwake.
 Mwili wa marehemu ukiingizwa katika Kanisa la KKKT Mtaa wa Kibwegere Kibamba kwa misa maalum,. Marehemu alikuwa akiimba kwaya ya Usharika huo.
 Waombolezaji wakiwa Kanisani hapo.
 Rafiki wa siku nyingi wa Ufoo Saro, Julieth Ngalabali kutoka gazeti la Mwananchi akiwa amebebna shada la maua na mwombolezaji mwingine.
 Wanahabari waliofika msibani hapo.
 Nje ya Kanisa hilo.
 Mwili ukiwa ndani Kanisani
 Waombolezaji wakiwa kanisani hapo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile ambaye wakati wa salamu zake alidai amemwakilisha Ufoo Saro ambaye yupo Hospitali na ameshindwa kuja kumuaga mama yake. Na amefanya hivyo kutokana na ombi la Ufoo.
 Mtoto wa Ufoo, Alvin Mushi akiwa na masikitiko na majonzi makubwa baada ya kuondokewa na Bibi yake. Alvin anadaiwa kulelewa na Bibi na Babu.
 Waombolezaji...
 Ilikuwa simanzi kubwa kwa Bi Joyce Mhavile boss wa Ufoo Saro.
 Mkurugenzi wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile akitoa heshima za mwishi. Picha ya juu ni mwana jamii.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho, picha ya chini ni wanakwaya wenzake na Marehemu.

No comments:

Post a Comment