Pages

Wednesday, October 16, 2013

MUNGU MKUBWA SHEKH SHARIF APONA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI


Kijana shekh sharif Khamis “16” ambae amekuwa kwenye kalama kubwa za mwenyezi mungu kwa dua zake katika ya wiki hii amenusika kifo baada gari yake kupata ajali mbaya kupelekea kuzunguka zaidi ya mara tatu na hali yake sio nzuri kutokana na kuumia nyonga ya mguu wa kushoto.
Akiongea kwa shida kwa njia ya simu namba 0717-688792 Shekh sharif alisema kuwa ajali hiyo iliwapata wakati wakitokea kijiji cha Mwailanje kuelekea Kiteto Mkoani Arusha na wakiwa wanaelekea kwenye majukumu ya kiimani huku gari hiyo ikiendeshwa na ustaadh Seif Othman na bila kutarajia alitokea mtoto akiwa anaendesha baiskeli kwa kasi mbele yao na dereva alipoona mtoto huyo anakaribia kuivaa gari kwa mbele ndipo alipomkwepa.
Hata hivyo Shekh huyo aliongeza kusema baada ya dereva wake kufanikiwa kumkwepa Yule mtoto ghafra upande uleule aliokwepea upande wa kushoto tairi la mbele lilipasuka upande ambao alikua amekaa shekhe huyo.
Baada ya kupasuka tairi hilo gari hiyo lenye namba za usajili T283 AJZ aina ya Lexus Aristi ilipoteza muelekeo na kupinduka zaidi ya ya mara tatu kama inavyoonekana kwenye picha ambapo baada ya hapo watu wote waliokuwemo ndani yake walitoka walipatwa na mshutuko huku shekh sharif mwenyewe akiuumia vibaya.
Akiongea mara baada ya ajali hiyo shekh huyo ambae amekuwa nchini na bara la afrika kwa ujumla kutokana mihadhara yake ya kuwaombea dua watu na kabla ya kuelekea mkoani Arusha shekh huyo alikuwa kwenye ziara za nchi za Burundi, Kongo, Angora na Zambia ambako huko alifanya mambo ya kushangaza kwa dua zake kuziombea amani nchi hizo zenye migogoro ya kivita.
Aidha katika hatua nyingine Shekh huyo mwanzoni mwa mwaka jana aliwahi kupata ajali nyingine kama hiyo ambayo gari yake ilitumbukia kwenye korongo na kukunjika kunjika kama chapati maeneo ya Morogoro lakini kwa kudra za mwenyezi mungu alitoka salama.


No comments:

Post a Comment