Katibu
mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani
iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo
mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na
wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara.
Alabama ni moja ya majimbo
yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake
ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita, viongozi wake walibuni
mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo
yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda, Mercedes Benz, Airbus,
Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na mengineyo Uchumi wake
unakua kwa kasi kubwa.
Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake
Dr. Slaa akimshukuru mmoja wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake
Kupitia
kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa alipata kukutana na
viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo ataweza
kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote,
Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana
na Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa miundombinu ikiwemo bandari,
ujenzi wa madaraja na bandari. Dr. Slaa na mkewe Josephine walipokelewa
na Gavana pamoja na mawaziri wake
Dr. Slaa, gavana na mawaziri wake wakiwa katika mjadala wa ushirikiano
Dr. Slaa Akimkabidhi Waziri wa Biashara Sera za Kiuchumi za Chadema
Dr. Slaa kwenye picha ya pamoja na gavana
Kubwa ya
yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza kuwa na ufanisi
hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita tu, huku
CCM ikiwapa walipa kodi wa Tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na kazi. Wengi
wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua sakafuni,
walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali duni na
wanafunzi wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa lililowakumba
watanzania
Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn
Kadhalika Dr. Slaa ametembelea
chuo kikuu cha auburn ambayo ni moja ya vyu vikuu vikubwa zaidi vya
utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli zake nchini Kenya, Uganda,
Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini Kenya, chuo cha auburn
inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa samaki na technologia
za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi kwenda ulaya Ulaya.
Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya ajira 7000.
Walipoulizwa kwa nini
walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena kwamba ni vigumu sana
kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa wangekuja na fedha zao
kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la USAID ambayo
inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya na
Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania ikiwa
mazingira ya kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala, ambayo
Mh. Slaa amewahakikishia kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao kazi.
Viongozi wa Auburn University
wako tayari kusaidia vyuo vya Tanzania kama Sokoine kwa kuwafundisha
waalimu na pia kubadilishana nao technolojia za kisasa za kilimo. Wako
pia tayari kuwafundisha wakulima wa aina zote na hata walaji mbali mbali
mbali.
Dr. Slaa akiwasili chuo kikuu cha Kilimo Cha Auburn. Nyuma yake ni walinzi kwenye msafara wake
Dr. Slaa
akiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa chuo cha kilimo kushirikiana na
vyuo vikuu vya tanzania kwa lengo la kubadilishana teknolojia na ujuzi
ili kuinyanyua kilimo cha tanzania na pia kuongeza ajira
Dr. Slaa akilakiwa na Dean wa Chuo cha Kilimo pamoja na viongozi wengine wa juu wa chuo hicho
No comments:
Post a Comment